Mfaham Ndege TAI {Eagle}
Tai ni moja kati ya aina ndege walio maarufu, Umaarufu wake umejikita katika mtindo wake wa maisha ambao ni wa kipekee.
Kuna aina nyingi wa Tai mfano; kuna tai mwenye mkia mweupe, kuna tai mwenye rangi ya dhahabu, kuna tai wa Ufilipino na kadhalika. Inakadiriwa kufikia aina sitini za tai duniani na wengi wao wanaoatikana Afrika, Ulaya na Asia.
Tai ni ndege aliye na sifa za upekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kwa sababu anaona Umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu.
Tai hukadiriwa kuweza kuishi zaidi ya miaka 60 na pindi afikishapo miska 50 makucha yake huwa yanakuwa yameshachoka, mdomo wake nao huisha makali.
TUANGALIE MAISHA YA TAI
Jambo la Kwanza
Tai hupaa juu sana angani wala shomoro na kunguru hawawezi kufika huko. Hakuna ndege yeyote mwenye uwezo wa kupaa juu sana kufikia kimo anachofikia. Mara nyingi huwa tunawaona mwewe wakipita sehemu fulani, shomoro na kunguru huwazomea lakini tai hataki ujinga huo.
FUNZO: Kaa mbali na shomoro na kunguru, Tai huruka na tai wenzie.
Jambo la Pili
Tai wanauwezo wa kuona mbali sana. wanauwezo kuona kitu kilichoko umbali wa kilometa tano. Tai akiona mawindo yake huangalia pale pale na huanza kwenda kukamata mawindo hayo kwa kasi kubwa. Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.
FUNZO: Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame mpake uyapate au uyatimize hiyo ndio siri ya kuelekea mafanikio yako, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe kaza mwendo bila kurudi nyuma.
Jambo la tatu
Tai hali mzoga, anakula kile tu alichokamata yeye.
FUNZO: Kuwa makini na kile unacholisha macho yako, masikio yako hasa kuangalia filamu na luninga. Usipende kutumia mizoga (mambo machafu) kwa sababu utaiharibu nafsi yako na maisha yako hatakwenda kwa kasi kubwa ya mafanikio.
Jambo la nne
Tai wanapenda mvua kubwa na yenye upepo. Mawingu yakikusanyika tai wanafurahi. Tsi hutumia upepo wa mvua kupaa juu sana hatumii nguvu nyingi kupaa anaweza kutandaza tu mabawa yake halafu anaanza kuelea bila shida akifurahia maisha mazuri. Huku ndege wengine wakati wa mvua kubwa yenye upepo hujificha kwenye mapango.
FUNZO:Tunaweza kutumia mvua kubwa yenye upepo(changamoto) kujinyanyua juu sana watu wote waliofanikiwa wengi wao hufanikiwa wakati wa changamoto kubwa. Wao hutumia mvua ya upepo kupaa juu sana angani tena wakati mwingine juu ya mawingu.
Jambo la tano
Tai hupima kwanza kabla ya kuamini. Tai jike akitaka kukutana na tai dume na wakataka kujamiiana, tai jike hupaa kwa kasi kubwa kwenda chini wakati huo tai dume anafuatia kwa nyuma. Akifika chini huchukua tawi la mti kisha hupaa tena angani na tawi hilo huku tai dume anafuata kwa nyuma. Akifika umbali mrefu angani tai jike huliachia hilo tawi na tai dumr hulikimbilia mpaka alikamate kabla halijadondoka chini na akisha likamata analirudisha tena juu kwa tai jike. Tai jike atalipokea hilo tawi na anapaa nalo juu sans halafu analidondosha tena. Kama kawaida yake tai dume atalifukuzia mpaka alikamate na atalirudisha kwa tai jike tena. Tai jike ataendelea na mchezo huu mpaka ajirizishe kwamba tai dume huyo yuko vizuri na amefuzu majaribio hayo. Hapo ndipo tai jike atakubali kupandwa na tai dume huyo jike.
FUNZO: Katika maisha yako binafsi au katika biashara au katika mapenzi yako, unatakiwa kupima mtu unayetaka kumpenda au kushirikiana naye kama kweli ana dhamira ya dhati au ni muogizaji tu.
Jambo la Sita
Tai akitaka kutaga mayai, tai jike na tai dume hushirikiana kutafuta sehemu iliyo juu sana kwenye mti ambayo sehemu hiyo haina maadui. Kisha tai dune anaenda chini ardhini kuchukua mitu yenye miiba anakuja anaitandaza kwenye sehemu wanayotengeneza kiota. Tai dume tena hurudi ardhini kuchukuwa matawi ya mitu kwa ajili ya kutengeneza kiota kikubwa. Kisha baada ya kuweka miiba na vimatawi vidogo vya mti, tai huyu anaenda tena chini kuchukua majani laini, akimaliza kuweka majani laini anatudi tena kuchukua miiba anakuja anaiweka juu ya kiota ili kuzuia maadui na mwisho akimaliza hayo yote ana nyonyoa baadhi ya manyoya yake ili kuweka sehemu ya mayai. Wanasaidiana na tai dume kuyaatamia kwa zamu, pia kazi ya ulinzi huifanya wote kwa kushirikiana. Vifaranga wakishatotolewa; tai dume na tai jike hushirikiana kuwalea. Baada ya muda kidogo tai jike ataanza kuwatoa vifaranga na kuwaweka kwenye miiba pembeni kidogo ya kiota, halafu vifaranga hurudi ndani ya kiota, atafanya hilo zoezi mara kadhaa baadaye atayaondoa manyoya kwenye kiota. Wale watoto wakirudi kwenye kiota watakutana na miiba itawachomachoma na kuvuja damu. Kisha tai jike atawarusha chini wale vifaranga kabla hawajadondoka tai dume atawadaka ataendelea na zoezi hilo moaka watoto wafahamu kuruka.
FUNZO: Pale tai wanapoandaa kiota wanatufundisha kujuandaa kwa ajili ya mabadiliko. Lakini ushiriki wa mke na mume ni muhimu sana ili kujenga familia yenye mafanikio.
Jambo la saba
Tai anapozeeka, manyoya yake huwa dhaifu na hayatamwezesha kupaa kwa kasi kama hapo zamani. Akiona hivyo huenda kwenye pango mbali na maadui, akifika humo kwenye pango hujinyonyoa manyoya yote hadi anabaki uchi kabisa. Anaendelea kujificha humo mpaka anaota manyoya mengine ndipo anatoka nje.
FUNZO:Wakati mwingine tunatakiwa kuziacha baadhi ya tabia mbaya ambazo zinatukwamisha kufikia mafanikio yetu makubwa.
View attachment 433068
0 Comments